Welcome to Tanzaniska Riksförbundet
(Monday - Friday)
Näsby Alle 6 183 55 Täby Stockholm - Sweeden

MKUTANO MKUU MALMÖ 2022

MKUTANO MKUU NA UCHAGUZI WA TANRIKS 2022

Uongozi wa Tanriks unapenda kuwajulisha Diaspora Watanzania kuwa, Mkutano Mkuu wa Tanriks 2022 utafanyika Malmö tarehe 26 Machi 2022. Uamuzi huo umefikiwa baada ya mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Tanriks uliofanyika tarehe 26 Septemba 2021. Mgeni rasmi ni Mhe.Balozi Grace Martin Olotu , Balozi wa Tanzania Nordic, Baltic na Ukraine na Mlezi wa Tanriks.

Kwa kuwa mkutano huo utakuwa na uchaguzi wa viongozi , Uongozi wa Tanriks unawa kumbusha wanachama kulipa Ada zao ili waweze kutimiza haki zao kwa mujibu wa katiba ya Tanriks. Unaweza kulipa Ada yako kupitia Swish 1230227694 – Tanzaniskariksförbundet , na kumjulisha Mtunza Hazina kwa simu +46760558079 , au kulipa Ada yako kidigital kupitia link hii Member Plan .

Kwa wale watakaohitaji msaada wa Tehama kukamilisha ulipaji wa Ada zao tunawaomba kuwasiliana na Mkurugenzi wa Tehama Eng. Jonathan Kayumbo simu + 46724511963 au kutuma barua pepe kwa admin@tanriks.com .

Taarifa hii ya awali ya Mkutano Mkuu inatolewa ili kuwawezesha Wanachama na Diaspora wengine kujiandaa mapema, kushiriki na kufanikisha Mkutano huu muhimu. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa, ikiwemo jinsi ya kushiriki katika kuchaguliwa katika uongozi kwa kadri zinavyokamilika.  Uongozi unawaomba wanachama kuendelea kutembelea tovuti yetu ya www.tanriks.com kwa taarifa zaidi kuelekea Mkutano Mkuu.

Tanriks inatanguliza shukrani kwa ushirikiano mkubwa mnao tupatia. Kusoma taarifa rasmi ya mwenyekiti , soma  hapa  MKUTANO MKUU 2022 TANRIKS

Asanteni.

TANRIKS INAWALETA WATU WOTE PAMOJA

Leave A Comment