Welcome to Tanzaniska Riksförbundet
(Monday - Friday)
Näsby Alle 6 183 55 Täby Stockholm - Sweeden

MIRATHI KWA DIASPORA NA WAGENI KISHERIA

 

MKUTANO MAALUMU WA TANRIKS KUJADILI MIRATHI KWA

DIASPORA NA WAGENI KISHERIA.

Baraza la diaspora wa Tanzania Sweden -Tanriks linawakaribisha wanachama na diaspora wote na familia zao, katika mkutano maalumu wa kujadilia haki za diaspora za urithi kupitia sheria ya mirathi ya Tanzania. Katika mkutano huo wanasheria wataufahamisha umma tafsiri ya mahakama kuhusu haki ya mirathi kwa mali zisizoamishika na haki nyingine kwa diaspora na familia zao lakini pia wageni wasiokuwa raia wa Tanzania.

Mkutano utafanyika siku ya Jumapili tarehe 14 August 2022, kuanzia saa 10 -12 jioni saa za Tanzania ambapo ni sawa na saa 9 – 11 Jioni saa za Sweden.  Watoa mada watakuwa ni Mwanasheria Alevander J. Barunguza na Mwanasheria Zakaria Maseke kutoka Tanzania. Nafasi ya kuchangia na kuuliza maswali kwa washiriki itakuwepo, washiriki mnaombwa kujiunga dakika 15 kabla ya muda wa mkutano ili tuweze kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.

Kwa msaada zaidi kuhusu mkutano huu WhatsApp namba +46724511963.  Taariza zaidi za kushiriki zinapatikana hapa chini, na kwenye tangazo hapo juu.  Kwa barua rasmi bonyeza hapa. MIRATHI KWA DIASPORA NA WAGENI KISHERIA Wote mnakaribishwa.

 

MKUTANO WA TANRIKS NA DIASPORA WOTE

MADA:  MIRATHI KWA DIASPORA NA WAGENI. KISHERIA

SIKU:  JUMAPILI TAREHE 14 AUGUST 2022.

MUDA: TANZANIA SAA 10 – 12 JIONI.  SWEDEN: SAA 9 – 11 JIONI

MAHALI: CLUBHOUSE.  JINA: TANRIKS DIASPORA

KUSHIRIKI: BONYEZA LINK HII – https://bit.ly/3oJzqNz   (KISHA BONYEZA ALAMA YA KALENDA ILI UWEZE KUKUMBUSHWA SIKU YA MKUTANO. )

WAZUNGUMZAJI. WANASHERIA WAWILI WALIOBOBEA KTK SHERIA ZA MIRATHI. UPATAPO TAARIFA HII, MTUMIE DIASPORA MWENZAKO.

 

TANRIKS INAWALETA WATU WOTE PAMOJA

 

Adolph N. Makaya

Katibu Mkuu
TANRIKS
2022 08 08

1 Comment

  • Merina Paul

    August 10, 2022 - 21:04

    I’m grateful for this enables people to be aware of legal issues

Leave A Comment